Tatizo Sio Ukosefu wa Ajira

Tatito la “ukosefu” wa ajira ni sugu katika jamii yetu. Inakadiriwa kuwa asilimia 12 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi hawafanyi kazi yoyote. Kutokufanya kazi ni tatizo kubwa zaidi kwa vijana ambao sio tu kwamba ndio wenye nguvu zaidi lakini ni wengi zaidi ya watoto na wazee.

201309250928180660Kwa mujibu wa takwimu zilizopo vijana zaidi ya 13% ya vijana wenye umri miaka 15-34 hawafanyi kazi. Na hata wale walioko kazini wanafanya kazi zisizokuwa na tija kama vile kilimo duni, vibarua, kazi za ndani na biashara za mikononi.

“Ukosefu” wa ajira unawakumba vijana wote – wasomi na wasiokuwa na elimu yoyote, wa kijijini na wa mijini wanawake kwa wanaume. Kila mwaka kuna vijana zaidi ya 800,000 wanaoingia katika soko la ajira na ni asilimia ndogo sana ya vijana hao wanaishia kupata ajira za maana. Inasadikika kuwa kati ya wasomi takriban 30,000 wanaohitimu katika vyuo vya juu nchini ni asilimia 5 tu wanaoajiriwa na wengine huishia mtaani.

Kama mtindo huu ukiendelea kwa kasi hii ifikapo mwaka 2030 watu wasio na kazi watafikia milioni 50.

Kuna sababu kongwe kadhaa zinazotolewa za watu kutokuwa kazini. Moja ya sababu hizo ni serikali kushindwa kuja na mkakati madhubuti wa kuwapatia vijana ajira. Sababu nyingine ni kwamba eti hakuna kazi kwenye soko la ajira- yaani wanaotafuta ajira wako wengi kuliko nafasi za ajira. Pamoja na kwamba sababu hizi zina ukweli ndani yake mimi nakataa kukukubali kwamba hizi ndio sababu kubwa (ama sababu za kweli) za tatizo la ajira nchini.

Kabla sijaendelea nataka niseme wazi kwamba kwa mtizamo wangu sababu kuu ya tatizo la watu kutokufanya kazi ni dhana potofu iliyojengeka kwa muda mrefu juu ya kazi na ajira. Kama tutakavyoona hivi punde tatizo haliko serikalini na wala si kweli kwamba nafasi za ajira ziko kidogo kuliko watafuta ajira . Ukweli ni kwamba nafasi za ajira ziko nyingi kuliko watafuta ajira.

Kwa muda mrefu serikali imekuwa muajiri mkuu. Nafikiri ndiyo maana wengi tumedhani kwamba ni jukumu la serikali kututafutia ajira. Lakini kwa mujibu wa tamaduni za jamii zilizostaarabika na zenye kujituma (na kwa mujibu wa kanuni ya Kibiblia pia) jukumu la kutafuta na kufanya kazi ni la mtu binafsi na sio vinginevyo.

Biblia inasema wazi kwamba mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi lakini hafanyi kazi hapaswi kula (2Thes. 3:10). Mtume Paulo alidiriki hata kusema kuwa Mkristo anayeshindwa kutunza familia yake ni mwenye dhambi kuliko mpagani (2Tim. 5:8). Maandiko hayamtetei mtu anayeishindwa kufanya kazi (au kutunza familia yake) kwa sababu kazi hazipo au kwa kuwa hajatafutiwa kazi (na serikali au vinginevyo)… La hasha. Mungu anasema yeyote asiyefanya kazi… akimaanisha kwamba nafasi za kazi siku zote zinakuwepo na kwamba ni jukumu la mtu binafsi kuitafuta angalau moja anayoiweza na kuifanya.

Baada ya kusema hivyo nigeukie sasa katika hoja yangu nyingine ya msingi – kwamba nafasi za kazi ziko nyingi tu ila tatizo ni uhaba wa watu wenye nia ya kuzitafuta au kuzifanya.

Ili tuelewane vizuri ni vema nitumie maneno ya Kristo mwenyewe kama yalivyonukuriwa katika Matayo 9:37 kwamba, “mavuno ni mengi lakini wavunaji ni wachahe…”

Kwa mujibu wa Kristo mavuno ni (watu wenye) uhitaji. Hii ina maana kwamba kazi (ajira) ni shughuli inayomletea mtu kipato (ujira) baada ya kukidhi uhitaji ama kuboresha maisha ya wengine. Kwa mfano unapotibu wagonjwa unapwaswa kulipwa.

Kwa maneno mengine kila uhitaji ni nafasi ya ajira au soko la biashara.

Kanuni ya kimungu inasema kwamba unapotumia raslimali zako kukidhi uhitaji au unapoboresha maisha ya wengine ni lazima tu utalipwa- bila kujali nani anakulipa. Kwa kuwa Mungu ndiye Bwana wa mavuno (wenye shida) kila unapofanya kazi (hata kama huna mkataba wa ajira) atahakikisha unalipwa tu.

Kama kila tatizo (uhitaji) ni nafasi ya kazi ndiyo maana Kristo anasema (namimi nakubaliana nae kabisa) kwamba nafasi za kazi ziko nyingi kuliko watu waliotayari kuzijaza hizo nafasi.

Tatizo tulilonalo ni kwamba wengi tunataka tuonyeshwe kazi , tuwe na mkataba, ahadi, ushahidi au uhakika wa ujira kwanza ndipo tuwe tayari kufanya kazi. Watu wanaopenda kuwa na uhakika wa ujira kwanza tatizo lao kubwa ni kwamba hawafanyi kazi vizuri na mara nyingi hukimbilia kazi nyepesi lakini zenye ujira mkubwa.

Kanuni ya Kiungu inasema kwamba thamani ya ujira siku zote inaenda sambamba na thamani ya kazi – yaani umuhimu wa uhitaji uliotatuliwa / kiwango cha ongezeko la ubora wa maisha.

Ujasiria mali ni kitendo cha ujasiri wa kutoa mtaji wako (wa ujuzi, pesa, muda, nguvu, au mali) kubuni, kutengeneza, au kusambaza bidhaa / huduma bila kuwa na ahadi kamili / mkataba / uhakika wa faida. Ujasiri huu unaitwa “risk” kwa lugha ya kiingereza. Hata mikataba mingi ya ajira ina “risks” zake – inatutaka tufanye kazi kwanza mshahara baadae.

Wajasiria mali wengi hutoa huduma kwanza kabla ya kupata faida. Utafiti unaonyesha kwamba wafanyabiashara mahiri hufilisika kwa wastani wa mara tatu katika kipindi cha maisha yao kabla ya kupata mpenyo wa kibiashara.

Wanamichezo mahiri wanalipwa mishahara minono kwa sababu wana dhihirisha ufanisi mkubwa kuliko wengine. Lakini ufanisi wao ni matokeo ya jitihada zao za awali katika mazoezi waliyoyafanya kwa muda mrefu kabla hawajapata mkataba wa ajira. Wanapodhihirisha / kuongeza ufanisi katika kazi ndipo wanapohalalisha mkataba / nyongeza ya kipato.

Kwa kifupi ni kwamba jamii yetu (hususan vijana) ni vema ielimishwe kuyaona matatizo (uhutaji katika jamaii ) kwa jicho la kibiashara zaidi. Ili kujipatia ujira ni vema kuangalia uhitaji unaoweza kuukidhi uliopo karibu nawe na kuingia kazini hata kama ni kwa kujitolea kwa kuanzia. Baada ya muda utashangaa jinsi gani milango itakavyofunguka. Jamii ni vema tukubali kwamba jukumu la kujiletea maendeleo kwa kujituma na kufanya kazi ni letu kimsingi. Kadhalika ni vema sote tuelewe kwamba kila mmoja wetu aliyehai ana uwezo wa kufanya kazi – yaani ana uwezo wa kutatua tatizo angalau moja katika jamii aliyopo. Tukifanya hivi naamini si tu kwamba tatizo la watu kutokufanya kazi litatokomea kabisa bali jamii yetu itaogelea katika bahari ya mafanikio, furaha na amani.

Kwa kuelewa hili huduma yetu ya Dream Life Mission imeanzisha mkakati kabambe wa kuwahamasisha wasiofanya kazi kujipatia ajira na kuanza safari ya kuelekea kwenye mafanikio yao mara moja. Ukihudhuria semina zetu utatoka na uwezo wa kujiamini na mkakati kabambe wa kujiajiri.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: