Juzi juzi nilikuwa napita mtaani nikakutana na wapendwa hawa wakiwa wanapumzika. Kusema ukweli ndugu zetu hawa hapa ndio ‘nyumbani’ kwao – hawana mahali pengine pa kuishi. Baada ya kuwaamsha na kuwasalimia kwa kifupi (sikutaka kuendelea wapotezea muda wao wa mapumziko) niliwapatia salamu zao za upendo kutoka kwa Muumba wao (ambaye pia ni Baba yetu sote!).
Wakati mwingine malalamiko,misongo ya mawazo na maumivu ya moyo hutoweka pale unapokutana na wengine wanaopitia kipindi kigumu kuliko wewe.
Ushauri wangu ni kwamba kama unajisikia kukosa raha kutokana na magumu unayopitia we nenda mahospitalini, kwenye misiba, kwenye vituo vya yatima au hata mtaani tu na kisha ongea na wahanga wa shida mbalimbali. Naamini ukitoka huko sio tu kwamba tatizo uliloenda nalo litakuwa limepata nafuu na kujifunza kuwa na shukurani kwa baraka nyingi ulizojaliwa na Muumba wako ambazo kwa sababu moja au nyingine hukuwa unaziona, bali utawiwa mzigo wa kutaka kufanya kitu ili kuboresha maisha ya wengine.
Bwana akutie nguvu. Amen