MBAPPE: SIRI YA USHINDI

mbappe.pngMashindano ya Kombe la dunia 2018 yaliyofanyika nchini Urusi yamekwisha. Kwa kukumbushia tu, timu ya taifa ya Ufaransa ilitwaa kombe kwa ushindi wa magoli 4 dhidi ya 2 ya wa-Croatia. Kylian Mbappe ( umri:miaka19) ni mmoja wa wachezaji walioiwezesha nchi yake kutwaa kombe la dunia kwa mara ya pili katika historia yao. Baada ya kufunga jumla ya magoli manne katika mashindano hayo (ikiwa ni pamoja na kufunga goli la nne katika fainali) Mpappe alitunukiwa tuzo ya mchezaji chipukizi bora katika mashindano hayo.

Wengi tunaufurahia umahiri wa Kylian Mpappe katika kusakata kabumbu, lakini ni wachache wetu tunafahamu siri ya mafanikio yake. Licha ya kuwa na kipaji; zaidi ya kuwa na bidii, nidhamu, kujituma katika mazoezi na kiu ya ushindani Mbappe ni mkarimu na mnyenyekevu.

Hata kabla ya mashindano haya ya Kombe la Dunia Mbappe (ambaye baba yake ni M-Camerron na mama yake ni M-Algeria) alikuwa patroni wa Premiers de Cordée – asasi inayo saidia watoto maskini na walemavu ili nao waweze kushiriki kimichezo.

Baada ya kuiwezesha Ufaransa kufikia hatua ya robo fainali kwa kuitoa timu ya Argentina Mbappe aliahidi kutoa posho yake yote atakayoipata kwa kushiriki mashindano hayo kwa Premiers de Cordée. Baada ya kutwaa kombe la dunia Kylian Mbappe alitoa takriban $500,000 ( Tsh bilioni moja) kwa watoto hao maskini. Alilipwa $ 22,300 kwa kila mechi aliyoshiriki na $ 350,000 kwa kutwaa kombe.

Akiuelezea moyo wa Kylian Mbappe baada ya kupokea taarifa za msaada huo, Mkurugenzi wa Premiers de Cordée Bw. Sebastien Ruffin alisema, “ Kylian ni mkarimu sana. Pamoja na kuwa na shughuli nyingi huwa anakuja mara kwa mara kuwaona watoto. Anapenda kucheza nao kwani inaelekea anawafurahia watoto kuliko wao wanavyomfurahia yeye. Kila anapokuja huwa na maneno muafaka ya kuwatia moyo kimaisha”

Kylian anaamini kwamba njaa ya mafanikio, bidii, nidhamu, ukarimu na unyenyekevu ni siri ya mafanikio ya kweli. Tunakwea kwenye kilele cha mafanikio kwa kushikana mikono na wengine wanaohitaji msaada wetu. Pamoja na kuwa tajiri na maarufu akiwa bado mdogo Mbappe bado ana kumbuka alikotoka. Anakumbuka wenzake ambao bado wanapitia maisha magumu ya mtaani alipokulia yeye.

Mafanikio ni dhamana . Mafanikio yetu ni fadhila tulizojaliwa na Mungu na ni wajibu wetu kulipa fadhila hizo kwa kuwasaidia wanyonge. Mungu hatasita kutumiminia mafanikio makubwa mara anapojiridhisha kwamba tutakuwa tayari kuwagawia wengine fadhili tutakazokirimiwa.

“… lakini nimekuombea wewe Petro ili imani yako isitindike, utakapofanikiwa wasaidie ndugu zako ” Luka 22:32

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: