THE TRANSFORMERS

Nephilim-Series-3-v.2Mungu ana kawaida ya kuwatumia watu wanyonge, wasiokuwa na uzoefu, waliodharauliwa na kutengwa ili kuleta ushindi mkubwa kwa Taifa.

Kwa mfano Daudi alikuwa kijana mdogo, aliyedharauliwa na familia yake kwa kuwa alizaliwa nje ya ndoa. Lakini ni Daudi huyu huyu aliyetumiwa na Mungu kumtungua Goliati na kuliletea taifa la Israeli ushindi mkubwa dhidi ya Wafilisti.

Katika pango la Adulam , mahali likokimbilia kujificha  dhidi ya Sauli, Daudi alifuatwa na watu takribani 400 waliokuwa na madeni, wasiokuwa na kazi wala makazi na waliokata tamaa. Daudi aliwafunza watu hawahawa  kuwa wanajeshi mahiri – jeshi  lililomuwezesha kuutwaa ufalme na ambalo halikuwahi kushindwa katika kipindi chote cha ufalme wake.

Gidioni alikuwa mdogo kuliko wote katika kabila dogo la Manase. Akiwa mtoto wa mwisho wa Mzee Joash, Gidioni alichaguliwa na Mungu kuwakomboa wana wa Israeli dhidi ya Wamidiani. Jefta ni kijana mwingine aliyetumiwa na Mungu. Akiwa miongoni wa watoto zaidi ya sabini wa Mzee Gilead Jefta alikuwa mtoto wa aliyezaliwa nje ya ndoa. Kwa maneno mengine alikuwa mtoto wa malaya. Na kwa sababu hiyo alifukuzwa nyumbani kwa mzee Gilead. Baada ya kufukuzwa nyumbani Jefta aliwakusanya vijana wengine waliokataliwa kama yeye na kuunda jeshi mahiri. Baadae Jefta alikuja kuwa Mfalme , sio tu wa ndugu zake waliomkataa, lakini wa Taifa zima la Israeli baada ya jeshi lake kuwapiga Waamoni.

Muda haunitoshi kuzungumzia habari za akina Musa, Yeremia, Joshua, Kaleb, Esta, Ruthu na wanawake wengine wengi ambao dunia ya wakati ule iliwadharau kiasi cha kutokujali hata kutaja majina yao.

Bwana hutumia vitu vinyonge ili kuviabisha vyenye nguvu. Mungu hutumia watu wachache na dhaifu ili tujue kwamba si kwa nguvu au uwezo wetu bali ni kwa Roho yake. Hivyo ndivyo Mungu anajiandaa kufanya katika nyakati zetu. Aanakusudia kuwatumia vijana wasiokuwa na sifa, uzoefu au majina makubwa ; wasio na tumaini, hadhi, kazi au makazi ili kuleta uamsho mkubwa wa kiroho na kufuta umasikini, rushwa na ubinafsi katika Taifa na Bara letu. Watu hawa tunawaita Life Transformers , au “ Transformers” kwa kifupi.

Huhitaji kuwa na vingi ili kutumiwa na Mungu. Kinachohitajika ni utayari wa kutumia nyenzo alizonazo na kutii maelekezo ya Mungu wako. Katika kipindi kifupi kijacho tutaanza fellowship na mikakati mingine ya kuwafikia waliopotea, waliokata tamaa , wahitaji na wenye shida. Kama unataka Bwana akutumie tuwasiliana nasi sasa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: