UKARIMU VS UTAJIRI

Can+I+Get+Money+From+Bill+GatesNiliipenda habari ya mtu aliyekuwa anafuatilia mahojiano katika moja ya vituo vya television huko Marekani. Ambapo tajiri nambari moja duniani Bilionea Bill Gates aliulizwa na mwandishi mmoja wa habari kuwa anajisikiaje kuwa tajiri mkubwa zaidi duniani. Akajibu kuwa hadhani kama yeye ni tajiri namba moja. Akaulizwa anadhani kuna mtu anamzidi? Akajibu “Nadhani yupo mmoja” Akaulizwa ni nani?

Akasema “Nilipokuwa shuleni sikuwa na fedha. Kuna wakati nilienda kwenye “vijiwe” vya kuuza magazeti ili nisome tu japo vichwa vya habari. Kijana mmoja mweusi (black American) ambaye alikua ombaomba eneo lile aliniona, alijua nilihitaji gazeti lakini sikuwa na uwezo wa kununua. Akatoa kiasi cha pesa katika zile alizokuwa amezikusanya katika harakati za ombaomba akaninunulia gazeti. Nilijaribu kukataa kwa sababu nilijua anaweza kulala njaa kwa sababu yangu, lakini alinisihi nichukue…

…Siku nyingine tena nilienda kijiwe kile na sikuwa na fedha. Sikutaka mtu yule anione. Hivyo nikapitia vichwa vya habari kimyakimya, na wakati naondoka nikaletewa gazeti, nimelipiwa na yule ombaomba. Akanitizama, akafurahi. Nikamtazama. Nikalia. Nikaondoka”

Mwandishi akamuuliza sasa huyo awezaye kuwa tajiri kuliko wewe wakati umesema ni ombaomba? Bill Gates akasema “mtu yule alitoa hata kile kidogo alichokuwa nacho ili kunisaidia. Hakujali kuwa anaweza kulala njaa, kukosa malazi, kukosa mavazi, hakujali kupoteza akiba yake yote ndogo aliyokuwa nayo ili kunisaidia. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi.”

Mwandishi akamuuliza, kwanini usimtafute umlipe? Bill akajibu. Nimeshamtafuta, nimemnunulia nyumba, na kumpa dola milioni moja (kama bilioni mbili za kibongo), lakini sijaweza kulipa hata robo ya alichonipa. Mwandishi akamuuliza kwanini? Bill akajibu “kwa sababu mimi nimetoa sehemu ndogo katika kikubwa nilichonacho, lakini yeye alitoa sehemu kubwa zaidi katika kidogo alichokuwa nacho. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi”

MASOMO:
1. Utajiri sio kiwango cha mali alizonazo mtu ; ni hali ya kuridhika na kiwango cha mali alizonazo.
2. Ukarimu hauna uhusiano wowote na kiasi cha mali alizonazo mtu. Kutoa ni utayari wa kukidhi uhitaji wa wengine kwa kutumia raslimali ulizonazo.
3. Kiwango cha furaha hakina uhusiano na utajiri. Lakini kiwango cha ukarimu kinaenda sambamba na kiwango cha furaha.
4. Kiwango cha ukarimu hakipimwi kwa kiasi kilichotolewa; ukarimu unapimwa kwa kiwango kilichobaki baada ya kutoa.
5. Ukarimu ni uwekezaji wenye uhakika wa faida kubwa.
6. Ukarimu unaambukiza, utafiti unaonyesha kwamba wakarimiwa huishia kuwa wakarimu kwa watu wengine angalau watatu.
7. Usimdharau mtu kwa kuwa leo hana hela ya kununulia gazeti , kesho anaweza kuwa tajiri kuliko wote duniani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: