HAPPY BIRTHDAY JESUS

Feed The Homeless Flyer - Made with PosterMyWallChristimas ni Birthday ya Yesu Kristo, mwaka huu anafikisha miaka 2018. Kama hivyo ndivyo ni vema nifikirie kumpa zawadi itakayo muenzi. Ili kujua ni zawadi gani itafaa kwenye Birthday ya Kristo ni vizuri kumuuliza Roho Mtakatifu anayemjua vizuri zaidi.

Nilipomuuliza nikanong’onezwa kwamba Kristo angependa kusherehekea na wasiojiweza, hususan watoto wasiokuwa na makazi.

Nilipoonyesha kushangazwa na chaguo la zawadi nilikakumbushwa kwamba Kristo mwenyewe hakuzaliwa hospitali au nyumbani, bali alizaliwa  mtaani , kwenye zizi la ng’ombe. Kimsingi Kristo alianza maisha kama mtoto wa mtaani. Mungu Baba yake alipanga mwanae azaliwe kwenye umasikini hivyo si kwa sababu hakuwa na uwezo au kwa kuwa yeye ni katili. Alitaka mwanae apitie umasikini ili aweze kuwahurumia masikini walio wengi.

Kristo alipozaliwa alihitaji matunzo ya kimwili ndio maana Mamajusi walimletea fedha na dhahabu. Lakini leo Kristo hahitaji pampas, kitanda ama maziwa. Christmas hii Kristo hatafurahishwa sana na hadhi ya mavazi , chakula, ama ibada yetu. Kitakacho mpa Yesu utukufu ni kuwajali masikini.

Tukiwalisha wenye njaa, tukiwavika walio uchi, tukiwanywesha wenye kiu, tukiwatembelea wagonjwa na na wafungwa, Kristo anasema, tutakuwa tumemfanyia yeye. (Matayo 25:35-36)

Dream Life Mission kwa upande wetu siku ya Christmas tumeamua kuwalisha na kuwanywesha watoto na vijana wanaoishi katika mitaa ya jiji letu la Dar-es-salaam.

Kama na wewe unampenda Kristo Christmas hii mpe Happy Birthday ya nguvu kwa kuwajali wenye uhitaji waliokaribu nawe.

Glorious Birthday Lord Jesus!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: