Hatimaye Kimbilio la vijana limepata makao rasmi. Kwa neema ya Bwana tumepata madarasa, mabweni, bwalo,jiko ofisi, store, vyoo, mabafu na visima vya maji. Yote haya yamejengwa juu ya kiwanja cha heka 4.
Kituo hiki cha Kimbilio kilichoko Mwasonga, Kigamboni Jijini Dar-es-salaam kitatoa huduma za makazi, afya,elimu, mafunzo, na ushauri katika masuala ya kimaisha, ajira, ujasiriamali, afya, uongozi na ushiriki katika maendeleo ya jamii.
Kama unavyoweza kujionea kwenye picha majengo na mazingira yanahitaji ukarabati wa kutosha kabla ya kuanza huduma zetu rasmi. Support yako ya hali na mali ni muhimu.