MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO

PLANE CRASH SURVIVORAntonis Mavropoulos alikuwa na muda mfupi sana wa kuunganisha ndege kwenda Nairobi kutokea Adis Ababa. Kutokana na kupotea mara kadhaa Antonis ambaye ni raia wa Ugiriki aliwasili dakika mbili baada ya muda wa kupanda ndege (check-in time).

Kwa kuwa alitakiwa kuwa Nairobi tayari kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa uliopangwa kuanza kesho yake Jumatatu Mavropoulos alisikitika sana kuikosa ndege yake hiyo aina ya Boeing 737 Max 8.

Mavropoulos alipatiwa ndege nyingine ya kuondoka asubuhi hiyo ya Jumapili tarehe 10.03.2019, lakini hilo halikupunguza jazba yake. Kwa hamaki iliyochanganyika na hasira Mavropoulos hakuelewa kwanini wafanyakazi wa Ethiopian Airline hawakumruhusu apande ndege yake hiyo licha ya kuwabembeleza sana.

Wakati anasubiri kupanda ndege yake mbadala jazba za Mavropoulos ziligeuka kuwa shukurani isiyokuwa na kifani. Hii ni baada ya kupata taarifa kwamba ndege iliyomuacha ilianguka na kuwaka moto dakika sita tu baada ya kupaa. Watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo Na. ET 302 walikufa papo hapo.

Ni mara ngapi tumehuzunika pale mambo yalipokwenda kinyume cha matarajio yetu. Ni rahisi kulaumu wengine, hali, mazingira au hata Mungu kwa kusababisha tukose kazi, tushindwe mtihani, tuugue au tuondokewe na wapenzi wetu. Mungu anajua yote na ana uwezo wote. Hakuna jambo linaloweza kutupata pasipo yeye kuliruhusu. Kwa kuwa Mungu anatupenda sana jambo lolote analoliruhusu katika maisha yetu ni kwa manufaa yetu makubwa zaidi.

Wakati mwingine, kama kwa kesi ya ndugu yetu Mavropoulos, Mungu hutupa nafasi ya kuzijua sababu zake nzuri za kuruhusu maumivu, lakini mara nyingi Mungu hatupi nafasi kama hiyo. Moja ya sababu ya Mungu kutotupa maelezo ni uwezo wetu mdogo wa kuelewa njia zake zilizo juu sana. Sababu nyingine ni kwamba Mungu ni Mungu, halazimiki kutolea maelezo kila jambo analoliamua.

Kama watoto wa Mungu anayetupenda upeo maandiko yanatuasa tushukuru nyakati zote, naam hata pale tunapopitia changamoto, (Wafilipi 4:4). Tunapaswa kufurahi hata katika maumivu tukijua kwamba mambo yote yanayotupata yamekusudiwa na Mungu kwa nia njema. Nirudie tena kusema, kila jambo, hususan yale mambo yanayoambatana na maumivu, hutufanya kuwa bora zaidi katika maisha haya ya sasa ama katika maisha ya umilele! (Warumi 8:28).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: