GIDEON RECRUITMENTS

four people holding green check signs standing on the field photographyTuko hapa kusajili na kutoa mafunzo kwa waalimu, walezi na washauri vijana watakao toa elimu, mafunzo, ushauri na huduma zingine muhimu kwa watoto na vijana wenzao masikini.

Kwa kushirikiana na shirika mama la Dream Life Mission, hususan kitengo cha Kimbilio lengo letu kuu ni kupunguza tatizo la ajira na umasikini kwa vijana nchini Tanzania.

Falsafa yetu ya kazi inasema: tumia raslimali zako kukidhi uhitaji wa wengine na kuboresha maisha yao. Maana yake ni kwamba kila uhitaji ni fursa ya kazi. Ukizingatia kwamba matatizo katika jamii yetu ni mengi sana ni wazi kwamba kuna kazi za kumtosha kila mtu.

Kama kweli unataka kutimiza ndoto zako na kuboresha maisha ya wengine – hususan watoto na vijana masikini – basi  jiandikishe hapa sasa. Baada ya kujiandikisha itakubidi uhudhurie na kufaulu Mafunzo Kazi kabla ya kuanza kazi yako rasmi.

Kama wewe  unatoa huduma kwa watoto na vijana masikini na unahitaji watenda kazi, Gideon Recruitments ni mahali pa kupata wafanyakazi waadilifu. Tafadhali tujulishe mahitaji yako hapa.

%d bloggers like this: