I assert that God – the creator of everything, the all-powerful, all-knowing, ever-present, with an independent superior will, and always in command – unconditionally love me and is the only one that deserves my worship.
I confess that Christ Jesus is the Lord , leader and perfect example. Due to His humbe sacrificial service God gave him authority over heaven and earth.
I’m gratefully aware that I’ve been wonderfully and uniquely made. God created me this way because He wanted to. He meticulously planned my life here on earth long before I was born.
I’ve been fashioned and sent to this world for a special purpose that involves improving lives in a unique way.
I accept that my wellbeing is tied to others. The quality of my life here on earth and in eternity is directly proportional to the value I add to the lives of others. Therefore, our collective prosperity is more important than my personal prosperity.
Since I matter to Him that much God will surely perfect His purpose in me.
I’m aware that part of this purpose – that is best and fully known by God alone – will demand my wilful participation to be fulfilled. In due course God will communicate His instructions to me and release the resources needed to execute them. My duty therefore is to always stay tuned to His voice and graciously yield.
I also know that God reserves the right to execute His plan in the manner that pleases Him. This means part of God’s purpose will be fulfilled in a way that defies my understanding, anticipation or preference. Since God is powerful, just and loving any circumstance He allows in my life is profitable to Him, and to us all.
After my life purpose on earth has been fully served I will go home to our Heavenly Father to start a new life in eternity.
Until then, I’m going nowhere. Nothing in heaven, nothing on earth or in hell; nothing in the past, present or in the future is strong enough to abort or alter God’s plan of love for my life.
Hence, I shall be at peace always. Yes, even in my pain, even during my darkest hour I’ll rejoice and praise God because He is ertenally good…!
Amen.
_________________________________________________
UKIRI WA IMANI
Namwamini Mungu – Muumbaji wa kila kitu, mwenye uwezo wote, ajuaye yote, aishie milele, mwenye mapenzi yasiyokoma, na mwenye enzi yote – aliyenipenda bila masharti na ambaye ndiye pekee anayestahiki kuabudiwa.
Nakiri kwamba Kristo Yesu ni mmiliki, kiongozi na kielelezo chetu. Kutokana na huduma yake ya kujitoa Mungu alimtunukia mamlaka juu ya mbingu, dunia na vyote vilivyomo.
Kwa unyenyekevu natambua kwamba nimeumbwa kiajabu na kipekee kabisa. Mungu aliniumba hivyo kwa utashi wake mwenyewe. Aliyapanga maisha yangu hapa duniani hata kabla sijazaliwa.
Nimeletwa hapa ulimwenguni kwa dhumuni mahususi la kuboresha maisha ya wengine kwa namna ya pekee.
Natambua kwamba mafanikio yangu yanatokana na mafanikio ya wengine. Thamani ya maisha yangu hapa duniani na kwenye umilele yanaenda sambamba na mchango wangu katika kuboresha maisha ya wasiojiweza hapa duniani. Kwa sababu hiyo mafanikio yetu sote ni ya muhimu kuliko mafanikio yangu binafsi.
Kwa kuwa Mungu anathamini sana kusudi lake juu ya maisha yangu ni lazima tu atatimiza kusudi lake hilo.
Natambua kwamba sehemu ya kusudi hili – ambalo ni Mungu pekee ndiye anaye lijua vizuri zaidi- itahitaji ushirikiano wangu wa makusudi ili kutekelezeka. Kwa wakati muafaka kwake Mungu atanipa maagizo na rasilimali nitakazozihitaji. Kwa hiyo, wajibu wangu ni kuwa makini kusikia sauti yake na kuwa tayari kuitii.
Najua pia kwamba Mungu Mwenye enzi ana haki ya kutekeleza kusudi lake kwangu kwa namna na wakati ulio muafaka kwake. Hii inamaanisha kwamba sehemu kubwa ya kusudi la Mungu litatimizwa kinyume na ufahamu ama utashi wangu. Kwa kuwa Mungu ni mwenye nguvu, mwenye haki na upendo mkuu chochote atakachokiruhusu katika maisha yangu kitakuwa cha manufaa kwake yeye, kwangu mimi, na kwa wengine pia.
Nikiisha kutimiza kusudi la maisha yangu hapa duniani nitarejea nyumbani kwa Baba yetu wa Mbinguni kuanza maisha mapya ya umilele.
Kama kusudi la Mungu juu ya maisha yangu halijakamilika sitaenda popote. Hakuna kitu chochote kilichoko mbinguni, duniani au kuzimu; hakuna kitu kilichotokea siku za nyuma, kinachoendelea sasa au kitakachotokea baadaye chenye uwezo wa kuizuia au kubadilisha upendo na kusudi jema la Mungu juu ya maisha yangu.
Kwa hiyo, siku zote nitakuwa na amani ya kutosha. Naam, hata wakati napitia changamoto, hata kama nina maumivu makali, hata pale ninapopita katika giza nene nitamfurahia na kumwabudu Mungu wangu kwa sababu ni mwema siku zote…!