WORK FOR GOOD NI NINI?
Kampeni ya vijana kujitolea kufanya kazi kwa watu binafsi, mashirika au taasisi.
MALENGO YA WORK FOR GOOD
- Kutunisha mfuko wa Kimbilio – mkakati wa kufuta umasikini na unyanyasaji wa watoto na vijana.
- Kuwapa vijana , hususan wasio na ajira, fursa, na uzoefu wa kazi na hivyo kuwaongezea uwezo wa kujipatia ajira ya kudumu.
- Kuwapatia waajiri wafanyakazi waadilifu kwa haraka, kwa muda wowote, na kwa gharama watakazo ziamua wao bila kufungwa na mikatababa ya kazi ya muda mrefu.
- Kutimiza agizo la Mungu la kuwajali wasiojiweza miongoni mwetu. (Waefeso4:28;Yakobo 1:27)
KAZI GANI ZITAFANYIKA
Tunategemea fursa za kazi kutoka kwa watu binafsi, taasisi, mashirika au makampuni binafsi
VOLUNTEER GANI TUNAOWAHITAJI
Tuna sajili na kuandaa volunteers wa kufanya kazi zote – kuanzia vibarua vya kukata majani, hadi kazi profesionals kama Ualimu na Uhasibu na Udakitari.
WORK FOR GOOD ITAANZA LINI?
Kampeni ya Work for Good itaanza rasmi tarehe 8 January 2019
MCHAKATO
Kabla ya kuanza kusambazwa katika vituo vya kazi volunteers watasajiliwa na kufaulu nadharia ya Mafunzo Kazi ili kuwajengea itikadi bora ya kazi. Zoezi hili linasimamiwa na Gideon Recruitments.
Awamu ya kwanza ya mafunzo itafanyika tarehe 31 December 2018.
Usajili sasa unaendelea na usajili utafungwa tarehe 23 December 2018.
NAMNA YA KUJISAJILI
Volunteers tafadhali jisajili hapa
Waajiri tafadhali sajili nafasi za kazi hapa
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi.